Jumatatu 25 Agosti 2025 - 21:22
Maonyesho ya Kimataifa ya Qur’ani katika jiji la Nantes, Ufaransa

Hawza/ Maonyesho yenye kuzingatia Qur’ani Tukufu yalianza tarehe 17 Mei katika jiji la Nantes, Ufaransa, na yataendelea hadi mwishoni mwa mwezi Agosti

Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, mpango huu unaoitwa “Qur’ani, Simulizi za Kiulaya” unafanyika katika Maktaba Kuu ya Jacques Demy na ni sehemu ya mradi wa kielimu uitwao European Qur’an (EuQu); mradi ulioanza tangu mwaka 2019 na umekuwa ukifuatilia nafasi ya Qur’ani katika historia ya fikra, utamaduni na dini barani Ulaya, katika zama za kati na mwanzoni mwa zama za sasa.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa kwenye tovuti rasmi ya mradi huu, watafiti wanajitahidi kufahamu jinsi Qur’ani ilivyotafsiriwa, kutarjumiwa, kunukuliwa na kutumika na Wakristo, Wayahudi wa Ulaya, wanafikra huru, wasiomuamini Mungu na pia Waislamu wa Ulaya katika historia, na athari gani imeacha katika tamaduni na dini barani Ulaya.

Katika maonyesho haya, nakala za maandishi na za kuchapwa za Qur’ani, mabango ya michoro, picha, kazi za sanaa na vitu vya kihistoria vimewekwa wazi kwa watazamaji, na wanao pendezwa navyo bado wana nafasi ya kuvitazama kwa siku chache zijazo.

Kabla ya kufika Nantes, mkusanyiko huu ulionyeshwa katika miji ya Vienna (Austria), Granada (Uhispania) na pia katika Maktaba ya Taifa ya Tunisia, na Nantes ikiwa mwenyeji wa mwisho wa maonyesho haya.

Mradi huu umetokana na ushirikiano wa kundi la watafiti mashuhuri wa historia ya dini; wakiwemo Mercedes García-Arenal kutoka Baraza Kuu la Utafiti wa Kitaaluma nchini Uhispania, Ian Loup kutoka Chuo Kikuu cha Kent, Uingereza, Roberto Tottoli kutoka Chuo Kikuu cha L’Orientale, Naples, Italia, na John Tolan kutoka Chuo Kikuu cha Nantes, Ufaransa.

Chanzo: http://www.al-kanz.org

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha